9 “Utatengeneza ua wa hema la mkutano. Upande wa kusini wa ua kutakuwa na vyandarua vilivyotengenezwa kwa kitani safi iliyosokotwa ambavyo vitakuwa na urefu wa mita 44 kwa upande mmoja.
10 Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
11 Hali kadhalika upande wa kaskazini, urefu wa chandarua utakuwa mita 44, na nguzo zake 20 za shaba, lakini kulabu za nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
12 Upande wa magharibi wa ua utakuwa na chandarua chenye urefu wa mita 22, na nguzo zake 10 na vikalio vyake 10.
13 Upande wa mashariki kuliko na mlango, ua utakuwa na upana wa mita 22.
14 Chandarua cha upande mmoja wa mlango kitakuwa na upana wa mita 6.5, pamoja na nguzo tatu na vikalio vyake vitatu.
15 Vilevile katika upande wa pili wa mlango chandarua kitakuwa mita 6.5, pamoja na nguzo tatu na vikalio vyake vitatu.