18 Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.”
19 Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia.
20 Lakini hutaweza kuniona uso maana hakuna mwanadamu yeyote atakayeniona na kuishi.”
21 Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kuna mahali karibu nami ambapo utasimama juu ya mwamba;
22 na utukufu wangu utakapokuwa unapita, nitakutia katika pango mwambani na kukufunika kwa mkono wangu, mpaka nitakapokuwa nimepita.
23 Halafu nitauondoa mkono wangu nawe utaniona nyuma, lakini uso wangu hutauona.”