24 Alikiweka kinara ndani ya hema la mkutano, upande wa kusini, mkabala wa meza.
25 Humo, mbele ya Mwenyezi-Mungu, akaziwasha taa zake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
26 Aliiweka ile madhabahu ya dhahabu katika hema, mbele ya pazia,
27 na kufukiza ubani wenye harufu nzuri juu yake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
28 Alitundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu,
29 akaweka hapo langoni mwa hema takatifu madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, akatolea juu yake sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
30 Aliliweka birika la kutawadhia katikati ya hema la mkutano na madhabahu, na kutia maji ya kutawadha.