1 Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia.
2 Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3 Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.
4 Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,
5 mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.”
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.