3 Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.
4 Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,
5 mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.”
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.
9 Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo.