4 Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,
5 mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.”
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.
9 Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.