1 Baada ya gharika, watoto wa Noa, Shemu, Hamu na Yafethi, walipata watoto wa kiume na wa kike. Hii ndiyo orodha ya wazawa wao:
2 Watoto wa kiume wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
3 Watoto wa kiume wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
4 Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu.
5 Hawa ndio asili ya watu walioenea sehemu za pwani, kila watu kwa lugha yao, kwa jamaa zao na kufuata mataifa yao.