21 Naye akamjibu, “Sawa, nimekubali ombi lako. Sitauangamiza mji ulioutaja.
22 Harakisha! Kimbilia huko, nami sitafanya lolote mpaka utakapowasili huko.” Hivyo mji huo ukaitwa Soari.
23 Jua lilikuwa limekwisha chomoza wakati Loti alipowasili mjini Soari.
24 Ndipo Mwenyezi-Mungu akateremsha moto mkali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora,
25 akaiangamiza miji hiyo, bonde lote, wakazi wake wote na mimea yote katika nchi hiyo.
26 Lakini mkewe Loti aliyekuwa nyuma ya Loti, akatazama nyuma, akageuka nguzo ya chumvi.
27 Asubuhi na mapema, Abrahamu alikwenda mahali alipokuwa amesimama mbele ya Mwenyezi-Mungu.