57 Nao wakasema, “Basi, tumwite msichana mwenyewe, tumwulize.”
58 Wakamwita Rebeka na kumwuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?” Naye akajibu, “Nitakwenda.”
59 Basi, wakamwacha Rebeka na yaya wake aende na mtumishi wa Abrahamu na watu wake. Yaya wake Rebeka pia aliandamana naye.
60 Basi, wakambariki Rebeka wakisema,“Ewe dada yetu!Uwe mama wa maelfu kwa maelfu;wazawa wako waimiliki miji ya adui zao.”
61 Kisha, Rebeka na wajakazi wake wakapanda ngamia na kumfuata huyo mtumishi wa Abrahamu; nao wote wakaondoka.
62 Wakati huo, Isaka alikuwa ameondoka Beer-lahai-roi, akawa anakaa huko pande za Negebu.
63 Siku moja jioni, Isaka alikwenda mashambani kutafakari. Basi, akatazama akaona ngamia wanakuja.