26 Watoto wa kiume wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27 Watoto wa kiume wa Eseri walikuwa Bilhani Zaawani na Akani.
28 Watoto wa kiume wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
29 Basi, hao ndio wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
30 Dishoni, Eseri na Dishani; kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake katika nchi ya Seiri.
31 Wafuatao ni wafalme waliotawala nchi ya Edomu, kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli:
32 Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.