2 Chemchemi za maji ya vilindi na madirisha ya mbinguni yakafungwa. Mvua ikazuiwa,
3 maji yakaendelea kupungua polepole katika nchi. Baada ya siku 150, maji yakawa yamepungua sana.
4 Mnamo siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
5 Maji yakaendelea kupungua polepole, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.
6 Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina,
7 akamtoa kunguru nje, naye hakurudi bali aliruka huko na huko mpaka maji yalipokauka nchini.
8 Kisha Noa akamtoa njiwa apate kuona kama maji yalikuwa yamepungua juu ya nchi.