4 Mnamo siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
5 Maji yakaendelea kupungua polepole, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.
6 Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina,
7 akamtoa kunguru nje, naye hakurudi bali aliruka huko na huko mpaka maji yalipokauka nchini.
8 Kisha Noa akamtoa njiwa apate kuona kama maji yalikuwa yamepungua juu ya nchi.
9 Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.
10 Noa akangoja siku nyingine saba, kisha akamtoa tena huyo njiwa.