6 Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina,
7 akamtoa kunguru nje, naye hakurudi bali aliruka huko na huko mpaka maji yalipokauka nchini.
8 Kisha Noa akamtoa njiwa apate kuona kama maji yalikuwa yamepungua juu ya nchi.
9 Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.
10 Noa akangoja siku nyingine saba, kisha akamtoa tena huyo njiwa.
11 Njiwa huyo akamrudia Noa saa za jioni akiwa na tawi bichi la mzeituni mdomoni mwake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua katika nchi.
12 Kisha akangoja siku nyingine saba, akamtoa tena yule njiwa; safari hii njiwa hakurudi kabisa.