3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,nami nitawaadhibu hao viongozi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4 Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:Watawala wa kila namna,viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,walio thabiti kama kigingi cha hema,wenye nguvu kama upinde wa vita.
5 Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitaniwatawakanyaga maadui zao katika tope njiani.Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
6 “Watu wa Yuda nitawaimarisha;nitawaokoa wazawa wa Yosefu.Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma,nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa.Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao,nami nitayasikiliza maombi yao.
7 Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani;watajaa furaha kama waliokunywa divai.Watoto wao wataona hayo na kufurahi,watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu.
8 “Nitawaita watu wanguna kuwakusanya pamoja;nimekusudia kuwakomboa,nao watakuwa wengi kama hapo awali.
9 Japo niliwatawanya kati ya mataifa,hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo.Nao pamoja na watoto wao wataishina kurudi majumbani mwao.