Mdo
Sura 5:15-21
Swahili Union Version
15hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.
16Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
17 Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,
18wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
19lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,
20Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
21Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha.Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.