47 Lakini Sulemani alimjengea nyumba.
48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,
49 Mbingu ni kiti changu cha enzi,Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu;Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana,
50 Au ni mahali gani nitakapostarehe?Si mkono wangu uliofanya haya yote?
51 Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo.
52 Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;
53 ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike.