8 Nao makuhani wakakubali kwamba wasipokee fedha kwa watu, wala wasitengeneze mabomoko ya nyumba.
9 Lakini Yehoyada kuhani akatwaa kasha, akatoboa tundu katika kifuniko chake, akaliweka karibu na madhabahu, upande wa kuume mtu aingiapo nyumbani mwa BWANA; na makuhani, waliolinda mlangoni, wakatia ndani yake fedha yote iliyoletwa nyumbani mwa BWANA.
10 Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
11 Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya BWANA,
12 na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya BWANA, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba.
13 Lakini havikufanywa kwa nyumba ya BWANA vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA;
14 kwa sababu hiyo fedha waliwapa watenda kazi, wakaitengeneza kwayo nyumba ya BWANA.