1 Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.
2 Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.
3 Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
4 Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya amiri huyu, ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA, Mungu wako; kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.