Ayu.
Sura 10:12-18
Swahili Union Version
12Umenijazi uhai na upendeleo,Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
13Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
14Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,Wala hutaniachilia na uovu wangu.
15 Mimi nikiwa mbaya, ole wangu!Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;Mimi nimejaa aibuNa kuyaangalia mateso yangu.
16 Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba;Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.
17Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu,Na kasirani yako waiongeza juu yangu;Jeshi kwa jeshi juu yangu.
18Kwa nini basi kunitoa tumboni?Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.