Ayu.
Sura 17
Swahili Union Version
Ayubu Aomba Apate Faraja
1 Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma,Kaburi i tayari kunipokea.
2 Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.
3 Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
4Kwani mioyo yao imeificha ufahamu;Kwa hiyo hutawakuza.
5Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
6 Amenifanya niwe simo kwa watu;Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi,Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
8Walekevu watayastaajabia hayo,Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.
9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake,Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
10 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.
11 Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika,Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.
12Wabadili usiku kuwa mchana;Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.
13Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu;Nikitandika malazi yangu gizani;
14Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu;Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;
15Basi, tumaini langu li wapi?Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?
16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,Itakapokuwapo raha mavumbini.