1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2 Enzi na hofu zi pamoja naye;Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3 Je! Majeshi yake yahesabika?Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5 Tazama, hata mwezi hauangazi,Wala nyota si safi machoni pake;
6 Siuze mtu, aliye mdudu!Na mwanadamu, ambaye ni buu!