Ayu.
Sura 10:17-22
Swahili Union Version
17Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu,Na kasirani yako waiongeza juu yangu;Jeshi kwa jeshi juu yangu.
18Kwa nini basi kunitoa tumboni?Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.
19Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo;Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.
20 Je! Siku zangu si chache? Acha basi,Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.
21 Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena,Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;
22Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo;Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote,Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.