8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga;Nawe utageuka na kuniangamiza?
9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,Na kunigandisha mfano wa jibini?
11 Umenivika ngozi na nyama,Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
12 Umenijazi uhai na upendeleo,Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
13 Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
14 Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,Wala hutaniachilia na uovu wangu.