Ayu.
Sura 10:9-15
Swahili Union Version
9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,Na kunigandisha mfano wa jibini?
11Umenivika ngozi na nyama,Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
12Umenijazi uhai na upendeleo,Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
13Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
14Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,Wala hutaniachilia na uovu wangu.
15 Mimi nikiwa mbaya, ole wangu!Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;Mimi nimejaa aibuNa kuyaangalia mateso yangu.