1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Hapana shaka ninyi ndinyi watu halisi,Nanyi mtakapokufa, ndipo na hekima itakoma.
3 Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi;Mimi si duni yenu ninyi;Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?
4 Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake,Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu;Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko.
5 Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau mashaka;Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.