Ayu.
Sura 12:15-21
Swahili Union Version
15 Tazama, yuayazuia maji, nayo yakatika;Tena, huyapeleka, nayo yaipindua dunia.
16Kwake yeye ziko nguvu, na makusudi kufanikiwa;Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.
17Yeye huwaondoa washauri hali wametekwa nyara,Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
18Yeye hulegeza kifungo cha wafalme,Na kuwafunga viuno vyao kwa mshipi.
19Yeye huwaondoa makuhani hali wametekwa nyara.Na kuwapindua mashujaa.
20Huondoa matamko ya hao walioaminiwa,Na kuondoa fahamu za wazee.
21Humwaga aibu juu ya hao wakuu,Na kulegeza mshipi wa wenye nguvu.