5 Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau mashaka;Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.
6 Hema za wapokonyi hufanikiwa,Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama;Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
7 Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha;Na nyuni wa angani, nao watakuambia;
8 Au nena na nchi, nayo itakufundisha;Nao samaki wa baharini watakutangazia.
9 Katika hawa wote ni yupi asiyejua,Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya?
10 Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake,Na pumzi zao wanadamu wote.
11 Je! Sikio silo lijaribulo maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?