1 Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamkeSiku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
2 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa;Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
3 Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye,Na kunitia katika hukumu pamoja nawe?
4 Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.
5 Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe,Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
6 Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,Wala machipukizi yake hayatakoma.