15 Wewe ungeita, nami ningekujibu;Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.
16 Lakini sasa wazihesabu hatua zangu;Je! Huchungulii dhambi yangu?
17 Kosa langu limetiwa muhuri mfukoni,Nawe waufunga uovu wangu.
18 Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka,Nalo jabali huondolewa mahali pake;
19 Maji mengi huyapunguza mawe;Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi;Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.
20 Wewe wamshinda nguvu sikuzote, naye hupita aende zakeWabadili sura zake, na kumpeleka aondoke.
21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui;Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.