Ayu.
Sura 14:16-22
Swahili Union Version
16 Lakini sasa wazihesabu hatua zangu;Je! Huchungulii dhambi yangu?
17Kosa langu limetiwa muhuri mfukoni,Nawe waufunga uovu wangu.
18Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka,Nalo jabali huondolewa mahali pake;
19Maji mengi huyapunguza mawe;Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi;Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.
20Wewe wamshinda nguvu sikuzote, naye hupita aende zakeWabadili sura zake, na kumpeleka aondoke.
21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui;Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.
22 Lakini mwili ulio juu yake una maumivu,Na nafsi yake ndani huomboleza.