4 Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.
5 Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe,Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
6 Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,Wala machipukizi yake hayatakoma.
8 Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani,Na shina lake kufa katika udongo;
9 Lakini kwa harufu ya maji utachipuka,Na kutoa matawi kama mche.
10 Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia;Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?