Ayu.
Sura 14:6-12
Swahili Union Version
6 Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,Wala machipukizi yake hayatakoma.
8Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani,Na shina lake kufa katika udongo;
9Lakini kwa harufu ya maji utachipuka,Na kutoa matawi kama mche.
10Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia;Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?
11Kama vile maji kupwa katika bahari,Na mto kupunguka na kukatika;
12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke;Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka,Wala kuamshwa usingizini.