1 Ndipo Elifazi, Mtemani, akajibu, na kusema,
2 Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio,Na kujaza tumbo lake na upepo wa mashariki?
3 Je! Ahoji na mazungumzo yasiyo faida,Au kwa maneno ambayo hawezi kufanya mema kwayo?
4 Naam, wewe waondoa kicho,Nawe wazuia ibada mbele za Mungu.
5 Kwani uovu wako unakufundisha kinywa chako,Nawe wachagua ulimi wake mwenye hila.
6 Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi;Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako.
7 Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa?Au, ulizawa wewe kabla ya milima?