11 Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako,Na hilo neno la upole si kitu kwako?
12 Mbona moyo wako unakutaharakisha!Na macho yako, je! Kwani kung’ariza?
13 Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu,Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.
14 Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi?Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
15 Yeye hawategemei watakatifu wake;Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.
16 Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu,Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
17 Mimi nitakuonyesha, unisikilize;Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;