16 Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu,Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
17 Mimi nitakuonyesha, unisikilize;Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;
18 (Ambayo watu wenye hekima wameyatangazaTokea baba zao, wala hawakuyaficha;
19 Waliopewa hiyo nchi peke yao,Wala mgeni hakupita kati yao);
20 Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote,Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.
21 Sauti za utisho zi masikioni mwake;Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;
22 Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,Naye hungojewa na upanga;