23 Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi?Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;
24 Mateso na dhiki humtia hofu;Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;
25 Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu,Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;
26 Humshambulia na shingo ngumu,Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;
27 Kwa kuwa amefunika uso wake na kunona kwake,Na kuwandisha mafuta kiunoni mwake;Naye amekaa katika miji iliyo ukiwa,
28 Katika nyumba ambazo hapana mtu azikaaye,Zilizokuwa tayari kuwa magofu.
29 Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu,Wala maongeo yao hayatainama nchi.