28 Katika nyumba ambazo hapana mtu azikaaye,Zilizokuwa tayari kuwa magofu.
29 Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu,Wala maongeo yao hayatainama nchi.
30 Hataondoka gizani;Ndimi za moto zitayakausha matawi yake,Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake.
31 Asiutumainie ubatili, na kujidanganya;Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake.
32 Jambo hili litatendeka kabla ya wakati wake,Na tawi lake halitasitawi.
33 Atayapukutisha mapooza yake kama mzabibu,Na kuyatupa maua yake kama mzeituni.
34 Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa,Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.