7 Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa?Au, ulizawa wewe kabla ya milima?
8 Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu?Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?
9 Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui?Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu?
10 Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi,Ambao ni wazee kuliko baba yako.
11 Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako,Na hilo neno la upole si kitu kwako?
12 Mbona moyo wako unakutaharakisha!Na macho yako, je! Kwani kung’ariza?
13 Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu,Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.