1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo;Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.
3 Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho?Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?
4 Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi;Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu,Ningeweza kutunga maneno juu yenu,Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
5 Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu,Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.
6 Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi;Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?