18 Ee nchi, usiifunike damu yangu,Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.
19 Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni.Na huyo atakayenidhamini yuko juu.
20 Rafiki zangu hunidharau;Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;
21 Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu,Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.
22 Kwani ikiisha pita miaka michache,Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.