7 Lakini sasa amenichokesha;Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.
8 Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu;Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.
9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;Amesaga-saga meno juu yangu;Mtesi wangu hunikazia macho makali.
10 Wamenifumbulia vinywa vyao;Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;Hujikutanisha pamoja juu yangu.
11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu,Na kunitupa mikononi mwao waovu.
12 Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja;Naam, amenishika shingo, na kuniponda;Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote,Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie;Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.