4 Kwani mioyo yao imeificha ufahamu;Kwa hiyo hutawakuza.
5 Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
6 Amenifanya niwe simo kwa watu;Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi,Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
8 Walekevu watayastaajabia hayo,Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.
9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake,Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
10 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.