9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake,Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
10 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.
11 Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika,Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.
12 Wabadili usiku kuwa mchana;Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.
13 Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu;Nikitandika malazi yangu gizani;
14 Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu;Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;
15 Basi, tumaini langu li wapi?Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?