1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2 Je! Hata lini utayategea maneno mitambo?Fikiri, kisha baadaye tutanena.
3 Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani,Tena kuwa wanajisi machoni pako?
4 Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako,Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe?Au jabali litaondolewa mahali pake?
5 Naam, mwanga wa waovu utazimika,Wala mwali wa moto wake hautang’aa.