5 Naam, mwanga wa waovu utazimika,Wala mwali wa moto wake hautang’aa.
6 Mwanga hemani mwake utakuwa giza,Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa.
7 Hatua zake za nguvu zitasongwa,Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
8 Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe,Naye huenda juu ya matanzi.
9 Tanzi litamshika kisigino chake,Na mtambo utamgwia.
10 Amefichiwa tanzi chini,Na mtego amewekewa njiani.
11 Matisho yatamtia hofu pande zote,Na kumfukuza karibu na visigino vyake.