1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini,Na kunivunja-vunja kwa maneno?
3 Mara kumi hizi mmenishutumu;Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu.
4 Ingawaje nimekosa,Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.