4 Ingawaje nimekosa,Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.
5 Kwamba mtajitukuza juu yangu,Na kunena juu yangu shutumu langu;
6 Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha,Na kunizingira kwa wavu wake.
7 Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi;Naulilia msaada, wala hapana hukumu.
8 Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita,Na kutia giza katika mapito yangu.
9 Amenivua utukufu wangu,Na kuiondoa taji kichwani mwangu.
10 Amenibomoa pande zote, nami nimetoweka;Na tumaini langu ameling’oa kama mti.