1 Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,
2 Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu,Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.
3 Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha,Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.
4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale,Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,