12 Ingawa uovu una tamu kinywani mwake,Ingawa auficha chini ya ulimi wake;
13 Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake.Lakini akaushika vivyo kinywani mwake;
14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika,Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.
15 Amemeza mali, naye atayatapika tena;Mungu atayatoa tumboni mwake.
16 Ataamwa sumu ya majoka;Na ulimi wa fira utamwua.
17 Hataiangalia hiyo mito ya maji,Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.
18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze;Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.