14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika,Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.
15 Amemeza mali, naye atayatapika tena;Mungu atayatoa tumboni mwake.
16 Ataamwa sumu ya majoka;Na ulimi wa fira utamwua.
17 Hataiangalia hiyo mito ya maji,Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.
18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze;Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.
19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini;Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.
20 Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake,Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia.